Book Name:Siyah Faam Ghulam

2. Uso wenye kung’ara

Sayyidna Asid Bin Abi Anas رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُ amesema, “Kuna siku moja Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم aliupitisha mkono wake juu ya uso wangu na kifua changu. Kwa Baraka yake nina poingia katika nyumba yoyote yenye kiza basi ile nyumba inang’ara.’ (Al-Kha_ais-ul-Kubra lis-Suyuti, juz. 2, uk. 142)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

3. Mwanga wa mwenye nuru

Ndugu wapenzi waislamu! Wakati Mtume mtukufu
صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم anaweza kuufanya uso na kifua kung’ara kwa kuupitisha mkono wake tu, je yeye mwenyewe
صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم atakuwa ana ng’ara kiasi gani? Imeelezwa katika Darimi kuwa Sayyiduna Abdullah Bin ‘Abbas
رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُمَا amesema, ‘Pindi Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akizungumza, ilikuwa ikionekana kama kuna nuru inang’ara kutoka kwenye mwaya wa meno yake ya mbele.’

(Sunan Darimi, juz. 1, uk. 44, namba. 58)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

 Total Pages: 37

Go To