Book Name:Siyah Faam Ghulam

na nimekubali kumtumikia Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ambae ameufanya uso wangu ung’are kama mwezi uliotimia. Katika ukaribu na yeye maumivu yote yanaondoka, madhambi yote yanafutwa na kiza cha ukafiri kinaondoka kabisa na wala hakuna ajabu ya uso wangu mweusi kubadilika ukawa ni mweupe wenye kung’ara.’

(imetolewa katika tafsiri ya Mašnawi, uk. 262)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Ndugu zangu waislamu! Maisha yangu nimeyatoa muhanga kwa ajili ya Mtume aliye barikiwa صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم. Allah! Allah! Aliashiria kwa maelezo kamili kuwa kuna mtu mwenye ngozi nyeusi anatembea na ngamia wake nyuma ya mlima, na amebeba ngozi ya kubebea maji. Kisha kwa uwezo aliopewa na Allah عَزَّوَجَلَّ aliwanywesha maji wasafiri wote mpaka wakatosheka na maji yaliokuwa kwenye ngozi hayakupungua hata kidogo na isitoshe Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akaupitisha mkono wake juu ya uso wa mtumwa mwenye ngozi nyeusi na akaung’arisha uso wake, bali mpaka  moyo wake uling'ara na akaingia katika Uislamu.

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

 Total Pages: 37

Go To