Book Name:Siyah Faam Ghulam

nilikuwa mkorofi sana kwa wazazi wangu. Kulikuwa hakuna tabia mbaya nilokuwa mimi sinayo. Baadae nikajiunga na jeshi na nikahama kutoka Rawalpindi kwenda Quetta. Wakati nipo njiani, nikawa ninawakera wasafiri wote katika treni. Nilipofika tu pale اَلْـحَمْـدُ لـِلّٰـه عَزَّوَجَلَّ nikakutana na kijana mmoja wa Dawat-e-islami. Alikuwa amevaa kilemba cha rangi ya kijani na alikuwa amehusiana na Gulzar-e-Taybah (Sargodha).

Akanifanyia juhudi binafsi na akaanza kunichukua kwenda katika jitimai za kushajiisha sunna ya kila wiki. Akaniathiri kwa tabia zake njema na nasaha zake maneno yake matamu. Nikatubia madhambi yangu yote yaliyopita nyuma na nikajilazimisha kukaa karibu ya mazingira ya madani, اَلْـحَمْـدُ لـِلّٰـه عَزَّوَجَلَّ zaidi nikapata shauku ya kusafiri pamoja na wafuasi wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم kwa muda wa masiku 30. Na sasa hivi niko kama msimamizi wa sehemu katika kitengo kimoja wapo nikifanya  juhudi ya kuwashawishi wengine kuzifanyia kazi sunna na kusimamimisha sala اَلْـحَمْـدُ لـِلّٰـه عَزَّوَجَلَّ.

Upendo kwa wacha mungu kunaleta thawabu ikiwa...

Ndugu waislamu! Mumeona! Kuwa pamoja na wafuasi wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم na kuwa na upendo kwa wacha

 Total Pages: 37

Go To