Book Name:Siyah Faam Ghulam

jambo hili kwamba mtu yeyote katika umma wako atakaekusalia mara moja, mimi nitamrehemu  mara kumi na yeyote katika umma wako atakae kusalimia mara moja, mimi nitamsalimia yeye mara kumi?’ (Mishkat-ul-Masabih, juz. 1, uk. 189, hadithi 928)

Mufti mwenye kutambulika Amad Yar Khan Na’imi
عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡـقَـوِی amesema, ‘Allah عَزَّوَجَلَّ, akimsalimia mja ina maana kwamba ima anawataka Malaika wamtolee salamu yeye au wampe hifadhi kutokana na majanga na mabalaa’.

(Mirat-ul-Manaji_, juz. 2, uk. 102)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Mtumwa mweusi

Kulikuwa na msafara unaosafiri katika bara Arabu. Msafara huu ukawa umeishiwa na maji yao na wakazidiwa na kiu kali sana mpaka walikaribia kupatwa na mauti lakini walibahatika kumuona Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akito kezea mbele ya macho yao. Wote walifurahi walipomuona yeye. Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم aliefunuliwa mambo ya ghaibu, alietakaswa na kila aibu akasema, ‘Nyuma ya mlima ule kuna mtumwa mwenye ngozi nyeusi anapita na ngamia wake. Analo gudulia la ngozi ndani yake kuna maji. Mwambieni aje na huyo ngamia wake.’

 Total Pages: 37

Go To