Book Name:Siyah Faam Ghulam

Kuandika  صbadili ya sala ya Mtume ni haramu

Sadr-ush-Shariah, Badr-ut-ariqah, ‘Allamah Mufti Muhammad Amjad ‘Ali Azami عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الـلّٰـهِ الۡـقَـوِی amesema, 'Ni faradhi (kwa muislamu) kumsalia Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم mara moja katika maisha yake. Katika mkusanyiko, ni wajibu kumsalia Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم muda wowote atakapotaja jina lake au kulisikia kutoka kwa mtu mwengine. Hata kama mtu atalisikia jina la Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم likitajwa mara mia moja katika mkusanyiko mmoja basi anatakiwa amsalie Mtume kwa kila mara atakayosikia. Atakaelisikia jina lenye Baraka na akawa hajamsalia basi anatakiwa amsalie hata baadae. Mtu atakaeandika jina lenye Baraka la Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni, ni wajibu kuiandika sala ya mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم pamoja na jina lake. Siku hizi watu wengi wanaifupisha sala ya Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم na wanaandkika, صلعم , عم,   ص ,    ع au (SAW) au (PBUH). Jambo hilo haliruhusiwi na ni haramu. Vile vile baadhi ya watu huwa wana andika   رض   na  رح    badala ya kuandika رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُ na رَحْمَةُ اللهِ تَعَالٰی عَلَيْه Jambo hili pia halitakiwi’

(Bahar-e-Shari’at, juz 3, uk. 101-102)

Unapoandika jina tukufu la Allah عَزَّوَجَلَّ basi uandike عَزَّوَجَلَّ au جل جلالہ  kwa ukamilifu.

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

 Total Pages: 37

Go To