Book Name:Siyah Faam Ghulam

Fadhila 8 za kupenda kwa ajili Ya Allah عَزَّوَجَلَّ

·         Allah عَزَّوَجَلَّ atasema katika siku ya Qiyama, ‘Wako wapi wale waliopendana kwa ajili ya utukufu wangu? Leo nitawaweka chini ya kivuli changu. Leo hakuna kivuli ispokuwa kivuli changu.(Muslim, uk. 1388, hadithi  2566)

·         Allah عَزَّوَجَلَّ anasema, ‘Mapenzi yangu yatakuwa ni wajibu (lazima) kwa wale wote wanaopendana wao kwa wao kwa ajili yangu na wakakaa kwa ajili yangu na wakakutana kwa ajili yangu na wakatumia pesa zao kwa kwa ajili yangu.’ (Al-Muwata, juzl. 2, uk. 439, hadith 1828)

·         Allah عَزَّوَجَلَّ amesema, ‘Wale wote wanaopendana wao kwa wao kwa ajili ya utukufu wangu kutakuwa na mimbari ya nuru kwa ajili yao. Mitume na mashahidi watawaangalia wao kwa pendo.’ (Tirmizi, juz. 4, uk. 174, hadithi 2397)

·         Ikiwa watu wawili watapendana wao kwa wao kwa ajili ya Allah عَزَّوَجَلَّ na mmoja akawa yupo kaskazini mwa dunia na mwengine akawa yupo mashariki basi Allah عَزَّوَجَلَّ atawaleta siku ya hukumu wote wawili na atasema ‘Huyu ndie uliyempenda kwa ajili yangu.’ (Shu’ab-ul-Iman, juz. 6,uk . 492, hadith 9022)

·         Peponi kuna nguzo za Yaqut(vito vyekundu) ambazo

 Total Pages: 37

Go To