Book Name:Siyah Faam Ghulam

kama utaratibu ulivyo katika Madani Qafla. Usiku watu walipolala, ndugu muislamu mmoja alipata bahati ya kumuona Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم kwenye ndoto akiwa ana furaha sana. Akabainaikiwa kama dawat-e-Islami ni harakati ya watu wema wanaoitangaza sunna na akawa amejitolea katika mazingira ya madani kimwili na kiroho. 

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Ndugu zangu wapenzi waislamu! Mumeona! Kwa baraka ya kuwa na pamoja na wapenzi wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم yule ndugu muislamu alipata bahati ya kumuona Mtume
صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم katika ndoto. Bila shaka suhuba ya wapenzi ina faida nyingi mno. Soma faida nyingine iliopatikana kwa baraka ya kusuhubiana na wapenzi wa Mtume  صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم na utafurahi.

Nilikuwa mpenzi wa filam za kigeni

Ndugu mmoja wa Kiislamu kutoka jeshini amesema: ‘Nilikuwa ninaongoza katika maisha ya dhambi na nilikuwa na kaseti mia moja za nyimbo. Nyimbo nyingi zilikuwa ni zenye maneno ya kukufuru مَـعَـاذَ الـلّٰـه عَزَّوَجَلَّ. Kuangalia filamu za kigeni ilikuwa ni jambo ninalolipenda zaidi. Kusikiliza nyimbo, vichekesho, kucheza karata, n.k. ilikuwa ni katika ratiba yangu ya kila siku. Nilikuwa ni mtu nisiejali kabisa naTotal Pages: 37

Go To