Book Name:Siyah Faam Ghulam

·         Kupeana mikono huondoa uadui.

·         Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم anasema, ‘Muislamu yeyote anaemsalimia mwenzake kwa kumpa mkono na pakawa hakuna hata mmoja anahisi uadui na mwenzake, Allah عَزَّوَجَلَّ atawasamehe madhambi yao wote wawili kabla ya mikono yao kuachana na yeyote anaemuangalia muislamu mwenzake kwa upendo na akawa hana uadui basi madhambi yao yaliopita yatafutwa kabla ya macho yao hayajaachana. (Kanz-ul-'Ummal, Juz. 9, uk. 57)

·         Mtu anaweza kupeana mikono na mwenzake kila wakikutana

·         Sio Sunna kupeana mikono kwa mkono mmoja. Sunna ni kwa mikono miwili.

·         Baadhi ya watu hupeana mikono kwa kupeana vidole tu;
jambo hili si katika Sunna.

·         Ni makuruhu mtu kubusu mkono wake mwenyewe. Walio na tabia ya kubusu mikono yao wenyewe baada ya kupeana mikono wajaribu kuepuka tabia hiyo. (Bahar-e-Shari'at, Juz. 16, uk. 115Mulakhkhasan)

·         Kama kupeana mikono na Amrad (mwanamume  anaevutia) kunasababisha matamanio basi hairuhusiwi kupeana nae mikono. Bali ikiwa kuangaliana nakoTotal Pages: 37

Go To