Book Name:Siyah Faam Ghulam

Lulu za madani 14 kuhusu kupeana mikono

·         Ni Sunna kwa waislamu wawili wanaposalimiana kupeana mikono.

·         Wakati wa kuaga ni sunna kuna kutoa salamu na kupeana mikono pia kumeruhusiwa.

·         Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم amesema kuwa waislamu wawili wanapo salimiana na wakaulizana hali zao basi Allah عَزَّوَجَلَّ huwatumia rehma mia moja baina yao. Rehma tisiini humshukia yule aliesalimia kwa bashasha zaidi kuliko mwengine na akaulizia hali ya mwenzake. (AL Mu'jam-ul-AWSAt, Juz. 5,uk 380., hadith 7672)

·         Marafiki wawili wanaposalimiana na kupeana mikono na wakamslia Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم basi madhambi yao yalopita na yajayo yatafutwa kabla ya hata hawajaachana  (Shu'ab-ul-Iman lil-Bayhaqi, Juz. 6, uk. 471, hadithi 8944)

·         Wakati muna salimiana mumsalie Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم na ikiwezekana musome dua hii pia يَغۡفِرُ اللّٰهُ لَنَا وَلَكُمۡ  (Allah عَزَّوَجَلَّ anisamehe mimi na wewe.)

·         Dua watakayo omba waislamu wawili wakati wakupeana mikono itajibiwa اِنْ شَــآءَالـلّٰـه عَزَّوَجَلَّ na watasamehewa kabla mikono yao haijaachana اِنْ شَــآءَالـلّٰـه عَزَّوَجَلَّ. (Musnad Imamu Ahmad Bin hanbal, Juz. 4, uk. 286,! hadithi12454)

 Total Pages: 37

Go To