Book Name:Siyah Faam Ghulam

Kukanusha elimu ya mtume kumesababisha kifo kibaya

Ndugu waislamu! Je, mumeona! Yule mtu hakuuthamini utukufu wa kuwa pamoja na kiumbe bora kuliko wote
hapa duniani. Akaritadi na akapinga elimu ya Mtume
صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم. Hatimae akafa kifo kibaya sana mpaka ardhi ikakataa kumpokea kabisa. Jambo hili linaonesha kwamba kukanusha elimu ya Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم kunachangia sana mtu kupoteza dira hapa hapa duniani na kesho akhera vile vile. Muislamu hawezi kabisa kukanusha elimu ya Mtume mtukufu  صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم, ni wanafiki peke yao ndio watakao kanusha. Kuna mtu mmoja amesema
اَلنِّفاقُ يُوۡرِثُ الاِعۡتِراض unafiki unarithisha ukanushaji.

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Ndugu waislamu! Mwisho wa maongezi yangu, ningependa kuchukua nafasi hii kuwatajia baadhi ya sunna na adabu. Mtume wa rahma, wa mwanzo kuingia peponi صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم amesema, ‘Yeyote anaependa sunna yangu basi amenipenda mimi na anaenipenda mimi atakuwa na mimi peponi.’

(Mishkat-ul-Masabih, juz. 1, uk 55, hadithi 175)

 Total Pages: 37

Go To