Book Name:Siyah Faam Ghulam

mpendwa صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم wewe omba dua na mimi nitawafufua.’ Basi Mtume wa walimwengu, tulizo la akili na moyo wetu, mkarimu na mwenye huruma صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akaomba dua na watoto wote wawili wakafufuka kwa amri yake Allah عَزَّوَجَلَّ. (Shawahid-un-Nubuwwah, uk. 105; Madarij-un-Nubuwwah,  juz. 1, uk. 199)

Aliemtusi mtume ametupwa nje ya kaburi

اٰمِيۡن بِجَاهِ النَّبِيِّ الۡاَمِيۡن صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلَيۡهِ وَاٰلِه وَسَلَّم

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Ndugu zangu wapenzi waislamu! Mumeona utukufu wa Mtume wetu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم! Chakula kidogo kiliwatosha watu wengi na hakikupungua. Kama haitoshi akasoma juu ya mifupa ya mbuzi na mbuzi yule akasimama akitikisa tikisa masikio yake. Vile vile akawafufua watoto wa Sayyidna Jabir رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُ kwa amri yake Allah عَزَّوَجَلَّ.

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Aliemtusi mtume ametupwa nje ya kaburi

Ndugu wapenzi waislamu! Sasa someni kisa chenye mazingatio cha mtu mbaya aliekanusha utukufu wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم.

 Total Pages: 37

Go To