Book Name:Siyah Faam Ghulam

12. Mtoto anafufuka

Mpenzi mkubwa wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ‘Allamah ‘Abdur Rahman Jami قُدِّسَ سِرُّ ہُ النُّوۡرَانِی anasimulia, ‘Sayyidna Jabir
رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُ alimchinja mbuzi mbele ya wanawe. Alipoondoka baada ya kumaliza, watoto wakachukua kisu na wakapanda juu ya dari la nyumba na mkubwa akamwambia mdogo wake, ‘Njoo! mimi nitakufanyia kama baba alivyo mfanyia mbuzi.’ Kaka mkubwa akaifunga mikono ya yule mdogo wake, akakipitisha kisu kwenye shingo yake na akamkata kichwa chake na akakibeba mkononi mwake. Mama yao alipoona akaja mbio na yule mtoto mkubwa nae akaanza kukimbia kwa hofu. Hatma yake akaanguka kutoka katika dari na akapoteza maisha. Mama aliekuwa mwenye subira licha ya kuwapoteza watoto wake wote wawili hakupiga mayowe na makelele kwasababu hakutaka kumsumbua mgeni wake mtukufu ambae ni rehema kwa walimwengu
صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم.

Kwa uvumilivu na subira ya hali ya juu kabisa akaileta miili ya watoto wake ndani ya nyumba na akaifunika kwa kitambaa na hakumwambia yeyote hata mume wake  Sayyiduna Jabir رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُ. Ingawa moyo wake ukawa unamwaga machozi ya damu, lakini aliendelea kutabasamu na kuonyesha furaha usoni mwake na akaendelea kuandaa

 Total Pages: 37

Go To