Book Name:Siyah Faam Ghulam

arubaini; kwa hiyo samaki huyu ataingia peponi.’ (Ruh-ul-Bayan, Juz.5,uk. 226, 518)

 

Wazazi waheshimiwa wataingia peponi

Ndugu Waislamu! Tafakarini tu! Samaki ambaye aliishi ndani ya tumbo lake siku chache Mtume wa Allah عَزَّوَجَلَّ Sayyidna Yunus عَـلَيْـهِ الـسَّـلاَم ataingia peponi, itawezekana vipi kwamba Bibi Aminah رَضِیَ اللهُ تَعَالٰی عَنْهَا afariki hali ya kuwa ni kafiri na aingie kaburini akaadhibiwe, wakati Bwana wa Sayyidna Yunusعَـلَيْـهِ الـسَّـلاَم Mtume Muhammad Mustafa صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم alibebwa katika tumbo lake kwa miezi kadhaa. Bila shaka wazazi wake wawili رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُمَا walitumia uhai wao katika kumpwekesha Allah عَزَّوَجَلَّ na ni miongoni mwa watu wa peponi. Aidha, mababu wote wa Mtume wetu mpendwa صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم walikuwa ni miongoni mwa watu wema. Kwa maelezo zaidi kuhusu hilo tafadhali kajisomee Fataawa Razawiyyah, juzuu ya 30, kutoka ukurasa 267 mpaka 305.


صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

11. Mbuzi aliekufa alihuika

Sayyidna Jabir Bin Abdullah رَضِىَ اللهُ تَعَالٰی عَـنْهُ mara moja alikuja kwa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akaona athari ya njaa katika uso wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم Muda huo huo akarudi nyumbani

 Total Pages: 37

Go To