Book Name:Siyah Faam Ghulam

nikawaona simba wengi wananinijia na wamefungua vinywa vyao wananguruma nawana saga saga meno yao, basi pakawa hapana njia yoyote isipokuwa kukimbia.’ Licha ya kuusikiliza muujiza huo, Abu Jahl akasema, ‘Hizo ni katika njama za uchawi za Muhammad.’ صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم (Allah عَزَّوَجَلَّ aepushe). (Al-Khasais-ul-Kubra lis-Suyuti, juz. 1, uk. 215)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

10. Wazazi wamefufuka

Kila mmoja anawapenda wazazi wake basi kwa nini Mtume Muhammad صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم asiwe na upendo huo kwa wazee wake! Kutokana na uwezo na nguvu alizopewa na Allah عَزَّوَجَلَّ Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم alifanya muujiza mmoja mkubwa sana ili awafanye wazazi wake kuwa katika umma wake. Basi soma kisa cha muujiza kifuatacho na ufurahi. Imam Abul Qasim ‘Abdur Rahman Suhayli (aliefariki mwaka  581AH) amenukuu ndani ya ‘Ar-Raudh-ul-Unuf’ kwamba Umm-ul-Mu’minin Sayyidatina ‘Aishah Siddiqah رَضِیَ اللهُ تَعَالٰی عَنْهَا anasimulia kwamba Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم aliomba dua, ‘Ewe Allah عَزَّوَجَلَّ! Wahuishe wazeee wangu.’ Allah عَزَّوَجَلَّ akaijibu Du’a ya Mtume wake صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akawafufua wazee wake kutoka makaburini. Wote wawili wakamuamini Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم na wakarejea makaribuni mwao.’ (Ar-Raud-ul-Unuf, juz. 1, uk. 299)

 Total Pages: 37

Go To