Book Name:Siyah Faam Ghulam

عَزَّوَجَلَّ nae ni mkarimu sana kwa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم kama anavyo mpatia ushindi dhidi ya maadui zake!

Kwa upande mwengine, Abu Jahl alieandikiwa kukosa fadhila za imani, akabaki vilevile na ukafiri wake licha ya ku ushuhudia muujiza kama ule kwa macho yake.

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

9. Simba wamefika

Isikilizeni simulizi hii yenye mafundisho ndani yake inayoelezea muujiza mwengine wa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم na upofu wa ndani kabisa wa Abu Jahl. Kwa kuwa Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم alikuwa akiwalingania watu kwenye uongofu, makafiri wa Quraishi wakaanza kuwa maadui zake na wakimuudhi yeye kwa njia tofauti tofauti. Kuna siku Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم alikuwa anapita katika bonde liitwalo hajun

Mmoja katika maadui aitwae 'Nadhr' akajitokeza mbele yake kutaka kumuua. Alipomkaribia Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم Nadhr akaanza kutetemeka na akakimbia kwa hofu kurudi mjini. Abu Jahl, baada ya kuona mkasa wote akamuulizia kilichomfanya awe vile. Akamjibu, ‘Leo nilimfuata Muhammad صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ili nimuue. Nilipomkaribia

 Total Pages: 37

Go To