Book Name:Siyah Faam Ghulam

akabisha hodi. Abu Jahl akauliza huku akiwa bado yupo ndani nyumbani, ‘Ni nani?’ jawabu  likatoka, ‘Muhammad.’ Abu Jahl akatoka, akashikwa na woga mkubwa sana. Akauliza,

‘Kimekuleteni nini hapa?’ Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم akasema, ‘Kwanini hujamlipa pesa yake?’ Akamjibu, ‘Ninamlipa sasa hivi.’ Basi, akazileta zile pesa na akamkabidhi mkononi yule mfanya biashara na akarudi nyumbani kwake. Watu wakamuuliza, ‘Abu Jahl ! Mbona ulikuwa na woga sana?’ Akawajibu, ‘Wakati Muhammad صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم alipotaja jina lake niliingiwa na khofu kubwa sana. Nilipotoka nilikiona kitu cha ajabu sana. Nimemuona ngamia mkubwa wa kutisha sana amesimama. Sijawahi kumuona hata siku moja maishani mwangu. Basi, nikahisi salama sana nimtii taratibu, kama si hivyo basi yule ngamia angenimeza.’

(Al-Khasais-ul-Kubra lis-Suyuti, juzuu . 1, uk . 212)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

Ndugu zangu wapenzi waislamu! اَلْـحَمْـدُ لـِلّٰـه عَزَّوَجَلَّ Ni mkubwa ulioje ukarimu wa Mtume wetu mpendwa, Mtume wa ulimwengu wote, tulizo la moyo, mkarimu na mwenye huruma صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم Namna gani alivyokuwa akiwasaidia wenye shida na matatizo na akiwasimamia waliodhulumiwa mpaka kupatiwa haki zao. Na pia AllahTotal Pages: 37

Go To