Book Name:Siyah Faam Ghulam

Vipi kuukanusha ubinadamu wa Mtume صَلَّی اللّٰہ تعالٰی علیہ واٰلہٖ وسلَّم?

Ndugu waislamau! Bila ya shaka, uhalisia wa Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ni Nuru, lakini tieni akiliini kwamba hairuhusiwi kabisa kuukanusha ubinadamu wake. Imam Ahmad Raza Khan عَـلَيْهِ رَحْمَةُ الـرَّحْمٰنْ amesema, ‘Kukanusha moja kwa moja ubinadamu wa mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ni  kufru (kukufuru).’ (FatawaRazawiyyah, juz. 14, uk. 358) Lakini ubinadamu wake sio wa kawaida, yeye ni bwana wa mabwana, ni mbora na mtukufu kuliko wanadamu wote.

Quran tukufu inasema:

قَدۡ   جَآءَکُمۡ    مِّنَ   اللّٰہِ    نُوۡرٌ   وَّ کِتٰبٌ   مُّبِیۡنٌ    ﴿ۙ۱۵﴾

Kwa hakika imekujieni nuru kutoka kwa Allah na kitabu chenye ubainifu.

(juz  6, Surah Al-Maidah, aya 15)

Katika aya iliyotajwa hapo juu, nuru ina maanisha kipenzi chetu Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم aliebarikiwa. Sayyiduna Imam Muhammad bin Jarir Tabari (aliefariki mnamo mwako 310 H) amesema; (صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلَيۡهِ وَاٰلِه وَسَلَّم) يَعۡنِيۡ بِالنُّوۡرِ مُحَمَّدًا: maana ya Nuru (ndani ya aya) ni Muhammad صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم.

(Tafsir-u-Iabari, juz. 4, uk. 502)

 

 Total Pages: 37

Go To