Book Name:Siyah Faam Ghulam

4. Kuta kung’ara

Inaelezwa katika shifaa: Kuta zilikuwa zinang’ara pindi Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم anapo tabasamu. (Ash-Shifa, uk. 61)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

5. Sindano iliyopotea

Sayyidatuna ‘Aishah Siddiqah رَضِیَ اللهُ تَعَالٰی عَنْهَا anasimulia, ‘Siku moja katika muda wa usiku nilikuwa nyumbani nikishona nguo basi ghafla sindano ikaniponyoka mkononi mwangu na taa ya mafuta ikazimika. Katika muda huo huo Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم mwenye nuru akaingia nyumbani, basi nyumba yote ikawa inang’ara kutokana na nuru ya uso wake na ile sindano iliyopotea ikaonekana.’ (Al-Qaul-ul-Badi’, uk. 302)

صَلُّوۡا عَلَى الۡحَبِيۡب           صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلٰى مُحَمَّد

سُـبْحٰـنَ الـلّٰــه عَزَّوَجَلَّ! Ni kung’ara kwa nuru kulikoje kwa Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم! Mufti mkuu mwenye kutambulika  Ahmad Yar Khan عَـلَيْهِ رَحْـمَةُ الْـمَنَّانْ amesema, ‘Mtume mtukufu صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ni Bashar (mwanadamu) vile vile ni nuru. Ina maana yeye Mtume صَلَّى اللهُ تَعَالٰى عَلَيْهِ وَاٰلِهٖ وَسَلَّم ni mwanadamu mwenye nuru. Kimwili ni mwanadamu na kiuhakika ni Nuru.’

(Risalah Nur ma’ Rasail-e-Na’imiyyah, uk. 39-40)

 Total Pages: 37

Go To